HIKI NDICHO ALICHOFANYIWA MWANAFUNZI HUYU NA MWALIMU WAKE
-Mwalimu wa kiume amtia vidole sehemu za siri
VITENDO
vya ukatili wa kijinsia na dhuluma dhidi ya watoto wa kike vimekuwa
vikishamiri kila siku pamoja na kuwepo kwa taasisi za kutetea haki za
wanawake na kuanzishwa kwa madawati ya Kijinsia kwenye vituo vya polisi nchini.
Msichana
wa kidato cha Nne mwenye umri wa miaka 17,(jina tunalo) anayesoma shule
moja ya sekondari ya Kata mkoani Mbeya amekumbwa na kadhia ya
kuchojolewa nguo zake za ndani na kucharazwa bakora zisizo na idadi na
walimu wanne wa shule hiyo.
Tukio hilo ambalo limeripotiwa katika kituo kidogo cha Polisi
Mbalizi wilaya ya Mbeya kwenye jalada la uchunguzi namba
MBI/IR/967/2016 na kuwekwa kwenye taarifa yenye namba MBI/RB/2653/2016
linadaiwa kuwahusisha walimu wanne akiwemo Mkuu wa shule hiyo pamoja na
walimu watatu.
Akizungumza
huku akiwa na maumivu makali katika Hospitali Teule ya Ifisi ambako
amelazwa akipatiwa matibabu, mwanafunzi huyo alisema kuwa aliitwa na
mwalimu wa nidhamu aliyemtaja kwa jina la Neema Mwaikenda aliyekuwa
pamoja na Mkuu wa shule hiyo aliyemtaja kwa jina la Mariamu Mwanisenga
na mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la Adili.
Alisema
walimu hao walianza kumuadhibu kwa viboko visivyo na idadi huku akiwa
amechojolewa nguo zake ambapo mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la
Adili akaanza kumshikashika sehemu zake za siri.
‘’Wakati naadhibiwa na walimu wote, huyu mwalimu wa kiume alianza kunishika huku
chini,na kunitaka niwataje wanaume zangu,nikawa nabana miguu wakazidi
kunishambulia kwa vibao na mateke na fimbo,’’alisema mwanafunzi huyo.
Alisema
sababu zilizosababisha aadhibiwe ilikuwa ni utoro na kuwa siku moja
alipokuwa shuleni alioneshwa na walimu fimbo na kuelezwa kuwa fimbo hizo
zitamuishia mwilini ndipo akaogopa kufika shuleni kwa siku tatu.
Anafafanua kuwa siku aliyofika shuleni ndipo alipokutana na kadhia ya kupigwa na walimu wanne hadi alipowaponyoka walimu hao na kukimbilia mitaani na kujificha.
‘’Niliwaponyoka
walimu nikakimbilia kwenye nyumba ya jirani na shule nikajificha hadi
jioni na baadaye kwenda nyumbani, kesho yake mama na dada walinichukua
na kunileta hospitali,’’alisema.
Mwandishi
wa habari hizi alifika shuleni anakosoma mwanafunzi huyo kwa nia ya
kukutana na uongozi wa shuleni hiyo ambapo Makamu Mkuu wa shule hiyo
aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwansanga alikataa kuelezea chochote.
‘’Mie
sijui lolote kwanza mie sio msemaji wa shule, kwahiyo sijui lolote juu
ya taarifa mnazohitaji,’’alijibu Makamu Mkuu wa shule na kuondoka zake.
Kwa
upande wake Ofisa Elimu wa Mkoa Charles Mwakalila alisema kuwa adhabu
aliyopewa mwanafunzi huyo ni kubwa kupitiliza kwa kuwa zipo taratibu za
adhabu kulingana na makosa na kuwa mwanafunzi anapaswa kupigwa viboko
vitatu na viboko visivyozidi sita au adhabu mbadala.
‘’Adhabu aliyopewa ni kubwa, tutafuatilia na waliokiuka taratibu watachukuliwa hatua za kinidhamu,’’alisema Mwakalila.
Naye
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari alipoulizwa juu
ya tukio hili alidai kuwa halijafika ofisini kwake na kuwa kwa sasa yeye
yupo kikazi wilayani Chunya na mara atakapofika ofisini atafuatilia na
kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika wa tukio hilo.
Awali
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mariamu Mtunguja ambaye alifika
Hospitalini alikolazwa mwanafunzi huyo alisema kuwa amemuangalia
mwanafunzi huyo na kuona namna ambavyo damu imevilia kwenye sehemu zake
za makalio na kwenye mapaja.
Mtunguja
alisema kuwa kitendo kilichofanywa na walimu hao ni cha kinyama ambacho
hakipaswi kuvumiliwa na kuwa mara itakapobainika atahakikisha walimu
hao wanachukuliwa hatua za kinidhamu