WENGER AITUPIA LAWAMA SAFU YAKE YA ULINZI

Kocha wa klabu ya soka ya Arsenal, mfaransa Arsene Wenger amesema kuwa pamoja na timu ya Bayern Munich kustahili pongezi kwa ushindi mkubwa wa magoli 5-1 dhidi ya timu yake, lakini anasema kuwa Arsenal iliwapa magoli mepesi mno wapinzani wao.
Tofauti na mechi ya awali Arsenal wakishinda goli 2-0 katika uwanja wa Emirates, jana usiku Bayern Munich walionekana kuyataka matokeo kwa nguvu zote.Wenger 2Akiongea mara baada ya mchezo huo, kocha Arsene Wenger amesema safu yake ya ulinzi ilikua mbaya sana hata kuruhusu magoli mepesi.
Arsenal iliyowakosa mlinzi Hector Bellerin na Laurent Koscienly ilipata wakati mgumu sana kuzuia mashambulizi ya Muller, Lewandowski na Arjen Robbean huku mlinzi Alaba naye akifunga goli moja zuri kwa uzembe wa safu ya ulinzi.
Wenger akasema kuwa kuelekea katika mchezo wao wa Jumapili wa ligi dhidi ya Tottenham Hotspurs, mlinzi Laurent Koscienly anatarajiwa kurudi lakini Hector Bellerin ataendelea kuuguza majeraha yake na kwamba Matheuw Debuchy ataendelea kucheza katika nafasi hiyo ya ulinzi wa kulia.Wenger 4Kuhusu matumaini ya kusonga mbele klabu bingwa Ulaya, Arsenal inatakiwa kushinda mechi zake zote mbili dhidi ya Zagreb na Olympiakos Pireus huku ikiombea Bayern wawafunge goli nyingi pia Olympiakos ili kuangalia uwezekano wa kufuzu hatua ya 16 bora.

TAFADHALI TUPE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.