SAMATTA AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO TP MAZEMBE KUCHEZA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA
TP Mazembe leo walifanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa fainali siku ya Jumapili November 8
Wachezaji wawili wa Tanzania wanaocheza kwenye klabu ya TP Mazembe wamejizolea sifa nyingi kwa kuiwezesha timu hiyo kufika hatua ya fainali. Umebaki muda mfupi watanzania hao kuweza kuandika historia mpya endapo watafanikiwa kuchukua kombe hilo.
Samatta amezungumzia changamoto aliyonayo kuelekea mchezo wa fainali hususan nafasi yake ya kuwania kiatu cha ufungaji bora wa ligi ya mabingwa barani Afrika.