OBAMA ATAKA GEREZA LA GUANTANAMO BAY LIFUNGWE
ikulu ya marekani white house imesema kua mipango ya kulifunga gereza la Guantanamo bay nchini cuba imefikia mwisho .Rais barack obama amelipa kipaumbele jambo hili tangu alipoingia madarakani mwaka 2009 lakin amekumbwa na vikwazo

Rais obama alitoa tamko la kirais kufungwa kwa gereza hilo lakini amekua akiwekewa vikwazo na baraza la congress ambalo lilikataa kuwahamisha wafungwa kwa hofu ya kiusalama

Wafungwa kadhaa wamejaribu kujitoa uhai kutokana mateso wanayopata gerezani humo
Wengi tayari wamerejeshwa nchini mwao japo kuna baadhi ambao wanaaminiwa kuwa ni hatari zaidi hawajaachiliwa