HAPPY OIL NA RUAHA FC WATOKA SARE MAVUNO CUP KILOSA

Ligi ya mavuno cup wilaya ya kilosa imeendelea tena leo katika viwanja vya azimio ambapo vigogo wawili wa ligi hiyo wenye tofauti ya point moja baada kucheza michezo minne minne  Happy oil kutoka magomeni wakiwa na point 8 na Ruaha fc kutoka ruaha wakiwa na point 7 wametimua vumbi katika viwanja hivyo ambapo timu hizo zimetoka droo licha ya happy oil kucheza pungufu baada mchezaji wa timu hiyo kupewa kadi nyekundu dakika ya 42 kipindi cha kwanza

Ligi hiyo yenye jumla ya timu 28 ambapo imekua ikichezwa katika sehemu mbili kilosa mjini na dumila,Huku kilosa kukiwa na timu 16 licha ya timu mbili kujitoa kwenye mashindano hayo kwasababu ya kushindwa kumudu gharama za usafiri
 Ligi hiyo yenye udhamini wa tsh milion kumi na moja ambapo mshindi wa kwanza atachukua milioni saba ,mshindi wa pili atachukua milioni mbili , mshindi wa tatu atajishindia milioni moja huku mchezaji bora atachukua elfu hamsini na mfungaji bora atachukua elf hamsini vile vile 



TAFADHALI TUPE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.