JIFUNZE JINSI YA KUANDIKA MISWADA YA FILAMU [SCRIPT]
Kuchagua idea ya story ya kuandikia script inategemea vitu kadhaa,kwanza bajeti ya yule unaye mwandikia na uwezo wa kiteknolojia,huwezi ukaandika kuhusu kuzama kwa mv Bukoba kwa mfano,maana imagination hazilipiwi hivyo unaweza kuandika chochote,lakini haitatendewa haki na yule unamwandikia.
Kingine usichague idea ambazo haupo mahiri na huru kwazo,mpaka pale utapo kuwa tayari kujifunza na kufanya risechi juu ya mambo yanayohusu idea hiyo,mfano kuhusu upelelezi! Kuandika movie ya kipelelezi lazima uwe na taarifa muhimu na halisia juu ya mambo ya kipelelezi na uwe na uwezo wa kuwa mbunifu kiupelelezi au upate mtu mwenye uwezo huo ahusike katika kuchangia ujuzi.
Idea sio lazima iwe na uhalisia,wa asilimia mia,japo inategemea ni aina gani ya uandishi unafanya,kama ni based on true sawa,lakini komedi na zingine sio lazima. Hapa naongelea pia katika mazungumzo ya kwenye script,dialogues ni kawaida zitofautiane na kua za kibunifu tofauti na zile za maisha halisi,maana dialogue za kwenye script zinakua na uhai zenye speed ya kutimiza lengo fulani wakati za maishani hazina haraka,kwa kuwa muda haubani wala budget,wala hazikaririwi,hivi ni muhimu mazungumzo yawe ya ubunifu wa kusisimua,na fupi lakini yenye lengo mahususi kuhusiana na story.
Lingine usiwe na haraka ya uandishi,jipe muda wa kufikiria na kuyapangilia mawazo katika mtiririko unaoeleweka. Kutimiza hili gawa story yako katika vipengele vitatu, 1. Utangulizi-hapa unawatambulisha wahusika na mahusiano yao,wasifu,pia chanzo cha kisa. 2. Mgogoro-hapa kisa kimetokea na namna kinavyoathiri wahusika. 3. Hitimisho-kisa kile kimeshaleta madhara,namna ya utatuzi umefanyika,wabaya wanalipwa,wazuri wanafaidika zaidi,mwisho Baada ya kufanya hayo yote,basi ni wakati muafaka wa kuandikika katika mpangilio unaokubalika na kueleweka,kumbuka ili kubuni na kuandika kitu kizuri,’MAZINGIRA’ yana influence kubwa kwenye fikra. Kaa mahali panapokufanya emotional na kukupa amani moyoni (mfano mimi napenda kuandika sehemu yenye upepo na juu kidogo,hii hunifanya kuwa na connection nzuri na hisia hasa pale ninapoandika kuhusu romance na maumivu),wengine hupenda kuandika kwenye chumba cha rangi flani,mfano,unaandika kuhusu maovu ukikaa chumba chenye mwanga hafifu kama nyeusi au nyekundu,au kusikiliza nyimbo za miondoko ya hip hop basi utakua inspired zaidi kupata idea za vurugu,huwezi kuandika romance ukiwa baa au mahali pa vurugu,wengine hupendelea kinywaji,mi nakubaliana nao lakini iwe kwa kiwango kidogo mno. Zipo software za bure na za kununua zitazoweza kukusaidia kufanya mpangilio automaticaly,mfano Montage,celtx,final draft n.k